Serikali yatolea Ufafanuzi Kupotea kwa zao la Pilipili Hoho


Thabit Madai, Zanzibar
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Hassan Khamis Hafidh amesema zao la Pilipili Hoho lilikuwa likizalishwa kwa wingi Zanzibar kwa kipindi kirefu na lilipotea kutokana na kukosekana soko la uhakika la bidhaa hiyo .

Hayo aliyasema kwa niaba ya Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani  wakati akijibu suala la Hidaya Ali Makame Viti Maalum Wanawake aliyetaka kujua kwa nini zao hilo limepoteza hadhi yake .

Alisema kukosekana kwa soko la uhakika la zao hilo  kwa kipindi kilichopita zao hilo lilipotea katika mazao ya biashara ambayo yalikuwa yanazalishwa vizuri kwa Zanzibar.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad