Sihofii Kutimuliwa Simba- Kocha wa Simba

Sihofii Kutimuliwa Simba- Kocha wa Simba
Kocha huyo aliyechukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuelezwa kutokuwa na maelewano mazuri na msaidizi wake, Mrundi, Masoud Djuma ambaye amemucha Dar katika mechi za mikoani wanazoendelea kucheza, huku pia matokeo yakionekana kutokuwa mazuri Msimbazi.



Akizungumza na Championi Jumatatu, Aussems amesema kuwa hawezi kuwa na hofu ya kutimuliwa kwenye timu hiyo kwa kuwa suala hilo ni kawaida kwa makocha.



“Niwe na hofu au niogope kufukuzwa kwa jambo gani labda ambalo linashangaza? Unajua kazi yangu ni kufundisha na walimu suala la kutimuliwa siyo geni, popote linatokea kwa wakati wowote, sasa nini kwangu cha kunifanya niogope?



“Kiukweli siwezi kuwa na hofu juu ya hilo, naijua vizuri kazi yangu ni ipi kama mwalimu, lakini tatizo limekuwa kubwa kwa sababu klabu nyingi za Afrika zimekosa malengo ya muda mrefu, ndiyo maana unaweza kuona ndani ya kipindi kifupi, timu inakuwa na makocha kibao ila imeshindwa kupata matokeo, hivyo ni jambo jema kuangalia malengo kama hayo anayotaka kufanya Mo (Mohamed Dewji),” alisema Aussems.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad