"Sijapata Mwanaume Kidume wa Kunitosheleza Kimapenzi" Rosa Ree


Rapa wa kike anayefanya vizuri na kibao chake cha 'one way', Rosa Ree amesema kwa sasa hayupo tayari kujihusisha kwenye mahusiano, kwa madai hajapata mwanaume ambaye ameweza kumpa changamoto za kuwa naye, kwani wengi waliojitokeza hajawaelewa.

Rosa Ree amebainisha hayo alipokuwa anazungumza na PLANET BONGO ya East Africa Radio na kusema kuwa na yeye ana ndoto ya kuja kuolewa siku moja lakini kwasasa hajaamua kujikita katika mambo hayo kwasababu alishawahi kuumizwa.

"Sio kwamba sijawahi kuwa katika mahusiano, nimeshawahi kuumizwa sana tu lakini kwa sasa ni kitu ambacho nimeweka pembeni nasio kwamba sihitaji mahusiano hapana. Kikubwa sijapata mwanaume ambaye atani-challenge, yaani mwanaume ambaye anaweza akawa dume, akanitisha hadi nikasema hapa kweli nimepata mwanaume", amesema Rosa Ree.

Pamoja na hayo, Rosa Ree ameendelea kwa kusema kuwa "sio kwamba anitishe au anipige hapana, ni vile awe na 'vission', 'intellegence', kwasababu nimetembea sehemu mbalimbali na kusumbuliwa na wanaume lakini ukiwaangalia vizuri unawaona kabisa hawajielewi".

Kwa upande mwingine, Rosa Ree amesema kutokana na muonekano wake watu wengi wamekuwa wakimfikiria vibaya kuwa pengine hawezi kujihusisha na mahusiano na kusahau kuwa na yeye ni mwanamke kama walivyokuwa wengine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad