Simba Yakwea Pipa Kuwafata Ndanda Mtwara

Simba Kuwafata Ndanda na Ndege
Kikosi cha Simba kinakwea ndege leo kuelekea Mtwara kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya Ndanda FC.

Mabingwa hao watetezi wa ligi wanaondoka leo jijini Dar es Salaam ambapo Jumamosi hii watakuwa wanacheza na walima korosho hao kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kuelekea mechi hiyo, uongozi wa Simba umesema asilimia kubwa ya maandalizi ya mchezo huo yameenda vizuri.

Aidha, Kocha Mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems, amesema dhamira yake ni kuchukua pointi 3 Mtwara hivyo ameahidi kuzipigania vilivyo ili kuiweka Simba kileleni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad