Sintofahamu ya Upinzani Bungeni Yamalizwa

Sintofahamu ya upinzani bungeni yamalizwa
Kutokana na hamahama ya wabunge wa upinzani kujiunga na CCM, hali ilyopelekea vyama walivyotoka kupoteza majimbo hayo, serikai imesema wabunge wa CCM kushinda katika majimbo hayo haihusiani na nafasi za wabunge wa viti maalum.

Hayo ameyasema Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde mapema leo Bungeni wakati akijibu swali la Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti maalum lililohoji juu ya nafasi za wabunge wa viti maalum waliopita kwa asilimia za majimbo yao.

Mavunde amesema kwa mujibu wa Ibara ya 78 ibara ndogo ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeainisha bayana kuwa wabunge wa viti maalum hupatikana wakati wa uchaguzi mkuu ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.

''Katika Majimbo ambayo wabunge wa upinzani wamehama na kujiunga na CCM na chama hicho kushinda kwenye majimbo hayo haiathiri idadi ya wabunge wa viti maalum kwa vyama vingine kwani idadi ya viti maalum hupatikana kupitia uchaguzi mkuu na sio uchaguzi mdogo'', amesema.


Wabunge wa majimbo mbalimbali yaliyokuwa yakiongozwa na vyama vya upinzani vyenye nguvu nchini wamekuwa wakijiuzulu na kujiunga na CCM, ambapo chama hicho tawala kimekuwa kikiibuka kinara katika chaguzi ndogo hivyo kuleta sintofahamu kwa wabunge wa viti maalum.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad