Siri za Matajiri wa Moshi Miaka ya 90 Hadi 2000's

Kipindi nakuwa moshi town pale wenyewe wanapaita mji wa wagumu, kulikuwa na matajiri wanajulikana na kusifika sana.
Walikuwa maarufu sana hadi makanisani.Ukienda kanisani ukimwona hata mke wake unabaki waooo
Walikuwa hadi na siti zao kristu mfalme pale.waliishi uzungun,wengine njia ya old moshi.

Kuna siku tumeenda nyumbani kwa rafiki yetu mmoja tulikuwa tunasomanaye mafundisho kanisan maeneo ya uzunguni kule,huo mjumba looh tulibak mdomo wazi.Na ilikuwa first time naona swimming pool nyumban.

Anyway zama zimepita, wengi wameaga dunia, wengine wapo ila umaarufu sio kama zamani. Nilikuwa natoka familia ya kikapuku kabisa so nilitaman siku moja at least na sisi family yetu iweze kuwa na jina kama family zile ama hata visenti tu.

Kuna mzee mmoja alikuwa maarufu sana hapo moshi town,alikuwa na maduka,garages,mabar,mabasi na biashara kibao.Alikuwa anaheshimika kama mfanyabiashara mkubwa moshi. Na wengi tuliamini hivyo.Bwana weeh siku moja katika harakati zake,akapatwa na majanga kwenye mbuga za Kenya, akapigwa risasi akafa,wenzie walifanikiwa kukimbia.Ikaja fahamika mzee alikuwa mwindaji haramu kwenye mbuga ya tsavo,alikuwa anawinda tembo na kuuza pembe na ndio ulikuwa siri ya utajiri wake.

Alirudishwa moshi akaenda zikwa kwao migombani ,after wards Mali zile zikayeyuka kama barafu. Since then nikajifunza kutokutamani cha mtu kwani hujui kakipataje. Matajiri wengi wa enzi hizo moshi na Arusha walikuwa wezi wa Magari Kenya na Madini...Utajiri una siri kubwa so vijana wenzangu tufanye kazi.

Usiamini story za nilianza na kushona viatu stend,huwa hawasemi ukweli.

By The Iron Batterfly

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad