Mwanadada Sister Fey ambae hapa karibuni aliwekwa rumande kutokana na kusambaza picha zisizokuwa na maadili wakiwa faragha na mpezni wake aliejulikana kwa jina la kisanii Holystar, wameamua kufunga ndoa na kuhararisha mahusiano hayo kimya kimya.
Ikiwa bado watu wanajua kuwa mwanadada huyo yuko Rumande , ghafla jana zilianza kusambaa picha zikimuonyesha mwanadada huyo akiwa katika vazi la harusi na mwanaume huyo wakiwa na furaha ya tendo hilo.
Hata hivyo mashabiki na wtu mbalimbali wanaamini kuwa kuna kitu kikubwa Sister Fey atakuwa amejifunza baada ya kuwekwa rumande na kukosa wa kumtetea kutokana na ukosefu wake wa maadili na kwa kufunga kwao ndoa basi watahshimu mahusiano yao.