Spika Ndugai Apiga Marufuku Wanawake Kubandika Kope na Kucha bandia

Spika Ndugai Apiga Marufuku Wanawake Kubandika Kope na Kucha bandia
Spika wa Bunge Job Ndugai amepiga marufuku wabunge wanawake kuingia bungeni wakiwa wamebandika kucha na kope za bandia.

Ndugai ametoa kauli hiyo bungeni leo baada ya Naibu Waziri wa Afya kujibu swali lililoitaka serikali kutoa elimu kwa watumiaji wa bidhaa hizo ambapo amesema kuwa “kwakuwa swali hili ni muhimu sana na kwakuwa mheshimiwa mbunge alitaka serikali ichukue hatua na mimi kwa mamlaka mliyonipa napiga marufuku wabunge kuingia humu ndani wakiwa na kucha bandia na kope bandia ili tuwe mfano”, amesema Ndugai.

Awali wakati Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile akijibu swali la Mbunge wa viti maalum (CCM) Fatma Tawfik lililohoji kuwa ni wanawake wangapi wamepata madhara ya macho kutokana na matumizi ya kope bandia ambapo amesema kuwa kucha za bandia na kope sio vipodozi kwa mujibu wa sheria ya chakula na dawa ya vipodozi.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa wagonjwa 700 hupokelewa na hospitali ya Taifa ya Muhimbili kila mwaka kutokana na kutumia vipodozi vyenye kemikali vikiwemo vidonge vya kubadili rangi zao za asili hivyo kupelekea ongezeko la saratani kutokana na matumizi ya vipodozi visivyotakiwa.

“Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA haina takwimu za madhara yatokanayo na matumizi ya kope bandia pamoja na kucha kwakuwa hatuna utaratibu wa kudhibiti bidhaa hizo kwa mujibu wa sheria”, amesema Dkt. Ndugulile.

Matumizi ya kucha bandia pamoja na kope yameshika kasi katika miaka ya 2010 na kuongeza ajira kwa baadhi ya vijana mitaani huku baadhi yao wakilalamikiwa kutotumia vifaa sahihi na kupelekea madhara kwa watumiaji wa bidhaa hizo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad