Steve Nyerere aijibu CCM Sakata la Kutemwa na Wasanii Kutemwa Kufanya Kazi za Chama

Steve Nyerere aijibu CCM Sakata la Kutemwa na Wasanii Kutemwa Kufanya Kazi za Chama
Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere amesema hawezi kubishana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally kuhusu kauli yake ya kutowatumia wasanii kwenye shughuli za kichama, kwa madai ana heshimu wanachokifanya na kukithamini.


Steve ametoa msimamo wake huo leo Septemba 03, 2018 alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv zikiwa zimepita takribani siku tatu tokea Dkt. Bashiru kutoa kauli ya chama hicho, kuwa kuanzia sasa hakitawatumia wasanii wa bongo fleva kwenye shughuli zao za chama na badala yake watatumia bendi yao ya TOT.

"Suala la Dkt. Bashiru sitaki kuliongelea kwa sasa, licha ya kuwa wamefanya kazi kubwa sana hivyo tuwathamini. Siwezi kubishana na Katibu Mkuu kwasababu yeye ana nafasi yake kwenye chama", amesema Steve.

Steve ambaye ndiyo kiongozi mkubwa katika shughuli za kichama kwa wasanii wa filamu na bongo fleva, amesema hawana mpango wowote wa kuanzisha kundi lao maalum la kuimba, kwa kuwa wanaheshimu maamuzi ya Katibu wao ila wapo tayari kufanya chochote watakachopangiwa.

"Tunasubiri maelekezo tu tutakayopatiwa na ndivyo tutafanya. Niwaombe wasanii wenzangu wote wanyamaze juu ya hili, tujipange na tusonge mbele kwasababu nia ni kuwaisaidia Tanzania. Tanzania kwanza hayo mengine baadae", amesisitiza Steve.

Wasanii wa filamu na bongo fleva walianza kutumika na Chama cha Mapinduzi katika shughuli za kichama hususan kampeni kwenye chaguzi kuu za Rais na Ubunge kwenye miaka ya 2005, ambapo kipindi hicho Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akitafuta nafasi ya kuingia Ikulu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad