Steve Nyerere: Sisi tunaheshimu mamlaka


Msanii wa filamu wa Tanzania na mchekeshaji marufu Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere, amesema kwamba kitendo cha wasanii kujihusisha na siasa kwa wakati mmoja, ni kitendo ambacho hakiwezi kuzuilika kwao kwani wao wanatii mamlaka, hata kama rohoni mwako hautaki. 

Akizungumza na wwww.eatv.tv, Steve Nyerere amesema kwamba suala la kufanya kazi za chama kwa wasanii kwanza wao wenyewe wanajiingizia kipato, lakini pia wanaheshimu na kutii mamlaka iliyopo ya uongozi wa nchi. 

“Sisi tunaheshimu mamlaka, mamlaka ambayo inaongoza ni ya chama cha mapinduzi, kuna muda unaweza ukawa rohoni mwako hautaki, usishindane na watu wenye nguvu, vyama vyama vinawahitaji kwa sababu wana nguvu kwenye jamii, sio kama sisi tunalazimisha, zamani tulikuwa tunaenda kwenye hafla za kiserikali sio kwenye chama, vyama vilikuwa na wasanii wao kina Komba, sasa hivi unajikuta unaambiwa bei gani unahitaji, utakataa!? Kwanza unalipwa na unaambiwa nenda, ukienda unakutana na CHADEMA, si lazima usifie waliokulipa!? Huwezi kukataa”, amesema Steve Nyerere. 

Kutokana na suala hilo Steve Nyerere amesema kwamba ni ngumu kuwatenganisha na siasa, kwani licha ya kwamba wao wanakuwa kazini, lakini pia kuna wengine ni makada wa vyama, hivyo wanapotumikia chama wanatakiwa watu waelewe kuwa wapo kazini 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad