TCU Imevifuta Vyuo Vikuu Viwili na Kusitisha Utoaji wa Mafunzo Katika Vyuo Vikuu Vitano


Imevifuta vyuo vikuu vya Teofilo Kisanji(TEKU) cha Tabora na Mtakatifu John(SJUT) cha Msalato Dodoma

Imeamuru wanafunzi waliokuwa wanasoma katika vyuo hivyo kuhamishwa kabla ya kuanza muhula wa mwaka wa masomo 2018/19
-
Aidha, TCU imesitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo vitano ambavyo ni Chuo Kikuu cha Mlima Meru, Chuo Kikuu cha Bagamoyo(UoB), Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga, Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (Arusha) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira(Bukoba)
-
Vyuo vingine 7 vimezuiliwa kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote. Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa.
-
Vingine ni SEKOMU, Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania-Kituo cha Marko na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania. - #regrann
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad