TID Atapa Pata... Aja na Mpango wa Kuuteka Tena Muziki

NA ELBOGAST MYALUKO
Wasanii TID a.k.a Mnyama na Kassim Mganga tajiri wa mahaba kutoka Tanga, wanajipanga kuuteka muziki wa 'Live' nchini baada ya kuweka wazi kuwa wanakamilisha mipango yao ya kuja na bendi ya pamoja.

 TID amefunguka hayo kwenye 'show' ya FNL inayoruka kila Ijumaa saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku kupitia East Africa Television ambapo alitambulisha ngoma yake mpya 'Washa' aliyomshirikisha Kassim Mganga.

''Nimeamua kuachia Audio kwanza kwasababu ina thamani kubwa na ninataka kurudisha muziki wa 'live' tupo kwenye mipango na Kassim tunataka kuja na band ili kuupa thamani tena muziki mzuri na sio kuwekeza kwenye video tu'', alifunguka Mnyama.

Mkali huyo wa kuimba na kucheza pia amefunguka kuwa 'Washa' ni miongoni  mwa ngoma zilizopo kwenye album yake ya 'The Vocalist' na ndio maana alikuwa kimya kwa takribani mwaka mzima tangu aachie ngoma inayoitwa 'Dada'.

Hata hivyo TID amesema tayari mipango ya 'kushoot' video ya Washa imeanza na muda wowote ataingia 'location' kwaajili ya kuwapikia chupa nzuri mashabiki wake huku akiahidi kuitambulisha kwenye FNL siku si nyingi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad