MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, amedai mchakato wa kulitoa shirika hilo kutoka mfumo wa analogia kwenda mfumo wa dijitali ulitokana na maelekezo ya rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Tido amesema hayo leo Alhamisi Septemba 20, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, alipokuwa akijitetea kuhusu tuhuma zinazomkabili.
Mtuhumiwa huyo akiongozwa na Wakili wake, Dk. Ramadhani Maleta, amedai TBC kutoka analojia kwenda dijitali, ilitokana na uamuzi wa Kikwete na kwamba alimtaka alibadilishe shirika hilo liwe na hadhi inayostahili na kwamba mchakato huo ulifanywa na bodi ya shirika hilo na kupata baraka za bodi ya zabuni.
Tido anakabiliwa na mashtaka manne yakiwemo ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia serikali hasara ya TSh milioni 887.1.
Tido Mhando Amtaja Kikwete Yake Mahakamani Kwenye Kesi
0
September 20, 2018
Tags