Trump Aishtumu China kwa Njama ya Kuingilia Uchaguzi wa Marekani

Trump Aishtumu China kwa Njama ya Kuingilia Uchaguzi wa Marekani
China inajaribu kuingilia uchaguzi wa katikati nchini Marekani , rais Donald Trump amewaambia viongozi wa dunian katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa.

''Hawanitaki mimi ama sisi kushinda kwa sababu mimi ndio rais wa kwanza kuipatia changamoto China katika maswala ya kibiashara , Trump alisema siku ya Jumatano.

Hatahivyo rais Trump hakutoa ushahidi wa matamshi yake . China na Marekani zimekua na mgogoro wa kodi tangu uchaguzi wa Marekani ufanyike.

Hatahivyo waziri wa maswala ya kigeni nchiniChina alipuuzilia mbali shutuma hizo. Uchaguzi wa bunge la Congress wa katikati wa muhula unatarajiwa kufanyika manmo tarehe 6 mwezi Novemba.

" Katika hotuba yangu kwenye mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa mataifa, nilitoa mpango wa utawala wangu wa kujenga amani katika siku zijazo'' , bwana Trump alisema alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa mjini New York.

''Na tunshinda katika biashara tunashinda katika kila kiwango. hatutaki waingilie uchaguzi wetu ujao''.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad