Tulia Ackson ni Mpinzani wa 'Sugu' 2020?


Tetesi zinasema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mbeya kimeonekana kuwa na imani kubwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dr Tulia Ackson kuwa anaweza kumng’oa Mbunge wa Chadema jimbo la Mbeya Mjini Chadema Joseph Mbilinyi kupitia Mbunge huyo wa kuteuliwa na Rais Magufuli.


Mbunge wa Mbeya mjini 'Sugu' akiwa na Naibu Spika wa Bunge Tulia Ackson.

www.eatv.tv imefatilia baadhi ya mwenendo wa matukio yaliyofanywa na Dr Tulia Ackson katika jiji la Mbeya kuanzia Julai 11 mwaka huu hadi septemba 20 ambapo wachambuzi wa siasa wanazitaja ni harakati za awali kuhakikisha C CM kinashika hatamu ya ubunge wa jimbo hilo ifikapo 2020.

Julai 12-2018 Dr Tulia Ackson alishiriki ibada ya kuombea amani ya jiji la Mbeya akiambatana na viongozi wa dini, machifu, na wananchi wa mbeya katika eneo la Ruanda Nzowe.

Julai 13-2018 Dr Tulia alitembelea soko la Kiwira Tandale, na alitoa msaada wa mifuko ya saruji 130 na matundu vyoo 26 kwa ajili ukarabati wa soko hilo.

Julai 14-2018 Alishiriki tuzo za walimu wanaofundisha shule za sekondari jiji la Mbeya.

Julai 15-2018 alianzisha mashindano ya ngoma za jadi TTDF na mashindao ya mpira wa miguu (Tulia Cup)  katika jiji la mbeya.

Julai 16  na 18 mwaka huu alitembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini, na hospitali ya teule ya mbalizi ambapo alitoa mashuka 30 na alikabidhi mabati 96 na mifuko ya saruji 80 kwa shule ya MNsingi Iwambi.

Julai 23-2018 akiwa na waziri wa Mwakyembe walizndua timu ya mpira ya miguu ya wanawake ya jiji la Mbeya. Julai 27-2018 alikabidhi mifuko 100 ya saruji kwenye kituo cha afya kata ya itezi.

August 01 na 27 mwaka huu Dr Tulia Ackson mifuko ya saruji 100 katika shule ya msingi mbeya mjini, pia alitoa msaada wa viti maalum kwa walemavu 17

Septemba 12 mwaka huu alitembelea vituo vya watoto yatima jijini Mbeya.

Septemba 20 hadi 22 hitimisho la tamasha la ngoma za jadi la Tulia Traditional Dance Festival ambapo mgeni rasmi ni Waziri mkuu Kassim Majaliwa.

Katika uchaguzi mdogo uliofanyika septemba 16 mwaka huu Chama hicho katika mkoa wa Mbeya kilishinda kata tano ikiwemo nne za Mbeya mjini ambapo ni Jimbo la Mbunge la Joseph Mbilinyi.

Www.eatv.tv ilimtafuta Mbunge Joseph Mbilinyi ili kupata maoni yake juu madai ya idara ya chuo vyo vikuu CCM mkoa wa Mbeya kuwa kiongozi huyo amepoteza mvuto alijibu kupitia ujumbe mfupi kuwa suala hilo haliwezekani.

“Hizo ni ndoto za alinacha, we si ni mwanahabari? njoo ufanye research (Utafiti) uone.” Aliandika Joseph Mbilinyi.

Www.eatv.tv imezungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Jakob Mwakisole amesema “…Chama hicho kina utaratibu wake wa kupata wawakilishi watakaowania nafasi mbalimbali za uongozi hivyo 2020 chama hcho kitapitia taratibu zake za kawaida..”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad