"Tuliingia Kwenye Meli Tukajiridhisha Kwamba Hakuna Alie Hai, Kwaiyo Tukasitisha Uokoaji" Mkuu wa Wilaya


Watu 44 wamepoteza maisha katika ajali ya pantoni iliyotokea katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Shughuli za uokoaji zinatarajiwa kuendelea leo baada ya kusitishwa jana usiku kutokana na giza.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali mkoani humo, mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika huku nahodha wa meli hiyo akiwa miongoni mwa waliofariki dunia.

Mwandishi wa BBC David Nkya awali alizungumza na mkuu wa wilaya ya Ukerewe Kanali Lucas Maghembe ambaye anasema kufikia wakati wa kusitishwa kwa juhudi za uokoaji Alhamisi jioni, waokoaji walikuwa wamechunguza ndani ya kivuko hicho na hakukuwa na dalili za kuwapata manusura wakiwa hai.

Amesema uchunguzi unaendelea na iwapo kulikuwa na utepetevu fulani uliosababisha ajali hiyo wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kanali Magembe amesema pia kwamba ikizingatiwa kwamba maeneo mengi eneo hilo ni maji, mfano Ukerewe ambapo maji ni asilimia 90, eneo hilo linahitaji meli na vyombo vingine vya usafiri ambavyo vipo katika hali nzuri
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad