Uchaguzi Mkuu Simba Kufanyika Novemba 3

Uchaguzi Mkuu Simba Kufanyika Novemba 3
Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba jana imeweka wazi tarehe ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza chini ya katiba mpya inayotambua mfumo wa hisa.


Kushoto ni msemaji wa Simba Haji Manara akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Boniphace Lihamwike (kulia).

Mwenyekiti wa kamati hiyo Boniphace Lihamwike ametangaza kuwa uchaguzi utafanyika Novemba 3, 2018 na taratibu za wagombea kuchukua fomu zinaanza mara moja.

''Uchaguzi utafanyika Novemba 3, 2018 na kesho jumatatu Septemba 3, 2018 tutaanza kutoa fomu kwa wagombea kwa nafasi zote na uchaguzi hivyo tunawaomba wenye sifa wajitokeze kwa wingi'', amesema Lihamwike.

Hatua ya Simba kuendelea na mchakato wa uchaguzi baada ya Vyama vya Michezo nchini kuisajili katiba mpya ya klabu hiyo inayoruhusu mfumo mpya wa uendeshaji.

Simba tayari imeshapata mwekezaji ndani ya klabu ambaye ni mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu Mo, aliyewekeza kwa asilimia 49 huku 51 zikisalia kwa wanachama.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad