Uchaguzi wa Monduli Mikononi mwa Polisi


Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limesema litaimarisha ulinzi katika uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge jimbo la Monduli unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili Septemba 16, 2018.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi,

Akitoa taarifa hiyo leo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi, amewataka wananchi wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupigia kura kwani usalama utakuwa wa kutosha.

“Kama ilivyo kwenye kampeni hali ilikuwa tulivu na wakati wa uchaguzi tutahakikisha kwamba hali hii inaendelea kuwa shwari, askari toka vikosi mbalimbali watakuwepo wilayani hapo kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya usalama.” Alilisitiza Kamanda Ng’anzi.

Kamanda Ng’anzi pia amewataka wananchi kurejea majumbani mara baada ya kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura kwani wakikaa kwenye vituo hali hiyo inaweza kusababisha vurugu.

Kwa wale wanaopanga kufanya fujo wakati wa uchaguzi au mara baada ya uchaguzi kumalizika Kamanda Ng’anzi amewaonya na kuweka bayana kuwa watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Katika uchaguzi huo wagombea wa CCM Julius Kalanga na yule wa CHADEMA Yonas Masiaya, wanachuAna vikali kuwania nafasi hiyo ambayo imekuwa wazi baada ya Julius Kalanga aliyekuwa CHADEMA kujiuzulu na kuhamia CCM.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad