Umoja wa Ulaya,China na Urusi Waitosa Marekani

Umoja wa Ulaya,China na Urusi Waitosa Marekani
Ulaya,Urusi na China zimejiweka katika nafasi ya kuvutana na rais wa Marekani Donald Trump baada ya hapo jana usiku kutangaza mipango ya kuunda njia maalum za kurahisisha shughuli za kibiashara na Iran,hatua ambayo inakiuka vikwazo vya Marekani.

Baada ya mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini kukutana na wajumbe kutoka Uingereza,Ufanasa,Ujerumani ,Urusi China na Iran hapo jana alitangaza kwamba nchi hizo ambazo zote zimesaini makubaliano ya Nuklia ya Iran zimefikia uamuzi wa kuendelea na shughuli za kibiashara na Iran.Akafafanua zaidi kwa kusema:

''Washiriki wamesisitiza haja ya kulinda uhuru wa uendeshaji wa kiuchumi ili kuwa na fursa ya kufanya biashara kwa njia halali na Iran kwa kuzingatia kwa ukamilifu azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa nambari 2231''

Maamuzi yaliyofikiwa na nchi hiyo yanamaanisha kwamba sasa Umoja wa Ulaya utaunda taasisi huru ya kisehria ambayo itaratibu shughuli kutowa na kupokea malipo ya fedha katika shughuli za kibiashara na Iran.

Mogherini aliendelea kusema kwamba kundi hilo la nchi Umoja wa Ulaya,China na Urusi  zimeidhinisha kwa kauli moja mapendekezo ya kiutendaji ya kuendelea kuzibakisha na kuziimarisha njia za kurahisisha mchakato wa malipo  yanayohusiana na biashara na Iran ikiwemo biashara ya mafuta.

Nchi zote zilizoshiriki katika mkutano uliofikia maamuzi hayo jana ziliafiki kwamba Iran inatekeleza majukumu yake kama sehemu ya mkataba wa Nyuklia uliosainiwa 2015 na hilo limethibitishwa katika ripoti 12 mfululizo zilizowahi kutolewa na shirika la kimataifa la Atomiki IAEA

Lakini hatua iliyochukuliwa na nchi hizo ni dhahiri inaweka mazingira ya kuzuka mvutano mkubwa na Marekani ambayo iliiwekea tena vikwazo Iran mnamo mwezi Agosti ambavyo pia vinataja kwamba nchi yoyote au makampuni yatakayoshirikiana kibiashara  na Iran yataadhibiwa. Duru nyingine ya vikwazo vya Marekani kuelekea Iran inatarajiwa kutangazwa mwezi Novemba na hasa vikilenga kukwamisha kabisa usafirishaji wa mafuta wa jamhuri hiyo ya kiislamu.

 Vikwazo hivyo vitamaanisha kwamba makampuni zaidi makubwa yatalazimika kuamua ama kuondowa vitega uchumi vyao Iran au kupoteza fursa zao za kibiashara na Marekani.

 Jana waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alifanya mkutano na waandishi habari akasema kwamba rais Trump atatumia nafasi yake kama mwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuzitolea mwito nchi zote kuunga mkono kampeini ya kuishinikiza Iran katika mpango wake wa Nyuklia.


 Uamuzi huo wa Marekani  lakini huenda ukasabababisha cheche za moto na wanachama wengine wa baraza la usalama la Umoja huo wa Mataifa,Uingereza,Ufaransa China na Urusi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad