Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho huwenda akatimuliwa kutokana na matokeo mabaya yanayoendelea kuikumba timu hiyo hatimaye Makamu rais wa mashetani hao wekundu, Ed Woodward ameonekana kutojali tofauti zilizopo na kumuunga mokono Mreno huyo kwakuwahidi kufanya usajili mkubwa ili kurejea kwenye makali yao waliyokuwa nayo hapo hawali.
Ed Woodward ameyasema hayo hapo jana kupitia mahojiano maalumu na mtandao wa Manchester United, huku mazungumzo hayo yakionekana kama kumuunga mkono Mourinho na kumtaka radhi baada ya meneja huyo mwenye umri wa miaka 55 kwa muda mrefu kuomba kupewa bajeti ya kusajili wachezaji wapya tangu mwanzo mwa dirisha la usajili wakati kiongozi huyo wa juu ndani ya klabu akishindwa kumuunga mkono kwa kutoa fungu hilo la fedha hali iliyotafsriwa kuwa wawili hao kutokuwa na mahusiano mazuri.
“Sisi ni timu kubwa ulimwenguni ambapo ukubwa wetu unaweza kuupima kwa idadi ya mashabiki tuliyonao, tunafahamu nafasi yetu ni lazima kuongeza juhudi na kuwekeza zaidi ili kuwa sawa,” amesema Ed Woodward.
Woodward ameongeza ”Bodi yetu, wawekezaji wetu na kila mmoja ndani ya klabu sawa na mashabiki tuna lengo moja kwa kile tunachohitaji kukifanya ndani ya uwanja ambapo ni kushinda taji na hiyo ndiyo sababu ya kumuajiri, Jose Mourinho na tayari ameshatupatia mataji matatu.”
Katika upande mwingine wachambuzi wa maswala ya soka akiwemo Alan Brazil anayeendesha kipindi cha michezo maarufu kwa jina la Breakfast wamemtafsiri kiungo wa Manchester United, Paul Pogba kuwa ndiye sumu ndani ya kikosi cha mashetani hao ambaye huwashawishi wachezaji wenzake kufanya matatizo.
Baada ya kushika nafasi ya pili mwishoni mwa msimu wa ligi kuu England bila ya kunyakuwa taji lolote wakiwa na pointi 19,Mourinho alihitaji kusajili wachezaji watano kwenye dirisha la usajili lakini iliwaambulia, Diogo Dalot, Fred na Lee Grant pekee huku ikichemka kuwapata Toby Alderweireld wa Spurs na Harry Maguire.