Update: Miili Iliyookolewa Ukelewe Yafikia 196

Update: Miili Iliyookolewa Ukelewe Yafikia 196
TAARIFA tulizozipata kutpoka katika Kisiwa cha Ukara ambako ndipo miili ya Marehemu inapelekwa kwa ajili ya kutambuliwa na ndugu zao, idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 196, miili 60 imeopolewa kwa leo hadi muda huu na uokoaji bado unaendelea.



Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018 na kwamba vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji na ikitarajiwa shughuli hiyo kufanyika hadi kesho Jumapili.



“Hadi jana (Ijumaa Septemba 21, 2018) miili 116 imeshapata ndugu na tunaamini miili mingine itatambulika maana wananchi wanaendelea kuwasili kuja kuitambua,” amesema Mongella.

Miili mingine 15 imeepolewa leo asubuhi na kufanya idadi ya vifo katika ajali ya MV. Nyerere kufika 151.

#MVNyerere: Baadhi ya ndugu ambao jana walikataa majeneza ya kuzikia jamaa zao waliofariki kwa ajali hiyo, wamebadili maamuzi yao na kuanza kudai wapewe majeneza. Mpaka sasa miili 116 imeshatambuliwa na ndugu. Zoezi la kuchukua miili litaendelea mpaka jioni.
08: 20HRS: Nahodha na Mkuu wa Kivuko cha MV Nyerere ni miongoni mwa watu waliofariki

Nahodha na Mkuu wa Kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi kikiwa safarini kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza, ni miongoni mwa watu waliofariki dunia katika ajali hiyo. Wengine ni fundi, mkuu wa kivuko, mlinzi na karani.

11: 00hrs: Idadi ya miili iliyoopolewa yaongezeka

Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 157 huku uokoaji ukiendelea.

11: 15 PM: MHANDISI WA KIVUKO APATIKANA AKIWA HAI

Mhandishi wa kivuko MV Nyerere, Alphonce Charahani ameokolewa akiwa hai siku 2 baada ya kivuko kuzama, amekutwa akiwa amejipaka oili mwilini. Sasa majeruhi wafikia idadi ya 41.



Zaidi ya wananchi 500 wamekwama katika eneo la Bugolora baada ya kukosa usafiri wa kuelekea kisiwa cha Ukara kulikotokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad