Updates: Mwili Mwingine Waonekana Ukielea Ajali Mv Nyerere


Mwili mmoja wa mtoto umepatikana saa nne asubuhi hii, wakati wazamiaji wakiweka sehemu ya chini Maputo (boya) yanayojazwa upepo ili kukiinua kivuko cha MV Nyerere, eneo la Bwisya kisiwani Ukara, jijini Mwanza.


Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho  kilichozama Alhamisi iliyopita na kusababisha vifo vya watu  225 ilianza jana  Jumamosi Septemba 23.

Kazi hiyo inafanywa na kampuni ya Songoro Marine chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara kilipozama kivuko hicho, mtaalamu kutoka kampuni hiyo, Meja Songoro alisema hatua ya kwanza itakuwa kuingiza hewa ndani ya kivuko ili kuyatawanya maji na kuanza kukivuta.

“Kivuko kinaendelea kuelea kwa sababu kuna hewa ndani yake. Wakati kinageuka (kupinduka) kilichota maji, tutaanza kuingiza hewa kutoa maji na kuanza kukivuta. Tutakapoanza kuyatawanya maji hayo, pia tutapeleka boya na hii itafanya chombo kizidi kuja juu. Baada ya hapo tutakisogeza taratibu hadi kwenye maji mafupi.” 
 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad