Upinzani Nchini DRC Watishia Kuandamana Kupinga Hatua ya Mahakama

Upinzani nchini DRC watishia kuandamana kupinga hatua ya mahakama
Chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimetishia kufanya maandamano na pia kutishia kuupinga uchaguzi mkuu baada ya mahakama ya juu kabisa nchini humo kusema mgombea wa chama hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais.

Jean-Pierre Bemba aliondolewa kwenye orodha ya wagombea nafasi ya uraisi baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha na mahakama kukosa imani na upande wa ushahidi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Baada ya kufanyika vikao vya ndani, chama hicho cha MCL kimetangaza rasmi kuwa kitatangaza baadaye tarehe rasmi ya maandamano hayo , kufuatia uamuzi wa mahakama ya katiba kuondoa jina la mgombea nafasi ya uraisi Jean-Pierre Bemba katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo.

Kwa muujibu wa chama cha MCL kimeyachukulia maamuzi ya mahakama hiyo ya katiba kama ya hovyo na yanayoweza kuiingiza nchi hiyo katika machafuko.

Katika taarifa ya chama cha Bemba, kimekitupia mzigo wa lawama tume ya uchaguzi pamoja na mahakama nchini humo kwa kuwa imejaa siasa jambo ambalo serikali imelipinga kwa nguvu zote.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad