Uwoya Atimba Kwenye Party Ya Wema na Mwarabu Fighter

Uwoya Atimba Kwenye Party Ya Wema na Mwarabu Fighter
SHUGHULI ilikuwa pevu pale kwenye Ukumbi wa Mlimani City MAMBO usiku wa Ijumaa ya Septemba 28, 2018 kufuatia Malkia Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu kufanya sheherehe ya kumbukumbuku ya siku yake ya kuzaliwa na mastaa kibao kujitokeza kumsapoti.

Mbali na birthday hiyo, Wema pia amezindua filamu yake yake ‘Day After Death’ aliyomshirikiana na staa wa filamu kutoka Ghana, Van Vicker.

Miongoni mwa waigizaji waliojitokeza kumsapoti Wema ni muigizaji mwenzake Irene Uwoya ambaye alishangaza watu kwa kuingia ukumbini hapo akiwa na aliyekuwa baunsa wa msanii Diamond Platnumz maarufu kwa jina la Mwarabu Fighter jambo lililoibua maswali iwapo baunsa huyo amehamia kumlinda Uwoya baada ya kutoswa na WCB.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad