Victiore Ingabire na Kizito Mihigo Waachiliwa Huru na Rais Kagame Rwanda

Victiore Ingabire na Kizito Mihigo waachiliwa huru na rais Paul Kagame Rwanda
Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu.

Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010.

Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa serikali na kudunisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Rais Uhuru Kenyatta asikia kilio cha Wakenya kuhusu bei ya mafuta
Amekuwa akiongoza ukosoaji wa rais Paul Kagame huku akiongezea kuwa hukumu yake ilishinikizwa kisiasa.

Bwana Kagame amepongezwa kwa kurekebisha uchumi wa Rwanda lakini pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu.

Kuwachiliwa huru kwa bi Ingabire na wafungwa wengine 2,140 kulitangazwa na seriikali kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri.

Taarifa ilisema kuwa bwana Kagame aliwaonea huruma chini ya uwezo wake kama rais.

Kwa nini baiskeli ni zawadi muhimu katika harusi Rwanda
Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa kwa miaka 10, 2015 kwa kupanga njama za kumuua rais Paul Kagame.

Alipokuwa akitoka jela, bi Ingabire alimshukuru rais Kagame, akisema huu ndio mwanzo wa kufunguka kwa sehemu ya kisiasa nchini Rwanda, kulingana na shirika la AFP.

Lakini waziri wa haki Johnston Businge alipuuzilia mbali umuhimu wa kuachiliwa kwa bi Ingabire.

''Hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kuachiliwa kwake-na hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kufungwa kwake'', aliambia Reuters.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad