Video inayoonesha Mateso Wanayopata Jela Yawaokoa Wafungwa Wakimbizi


Wahamiaji wa Nigeria waliokuwa wanashikiliwa katika selo za polisi nchini Libya wamefanikiwa kujiokoa baada ya kujirekodi video fupi inayoonesha wanavyoteseka na kuisambaza.

Wakijua kuwa ni hatari zaidi kukutwa na simu ndani ya selo hizo, mmoja wa washikiliwa aliyekamatwa akijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya, alijitoa mhanga akiwashirikisha baadhi ya wenzake.

“Wamekataa kuturudisha kwetu, wanatutesa, tunakufa huku… wanatuweka hapa kutufanyia biashara  ya utumwa,” wanaonekana wafungwa hao kwenye kipande cha video ambacho kilisambaa kwa kasi kwenye Whatsapp.

 Kipande hicho cha video kinachoonesha mazingira mabaya na hatari ndani ya selo hizo inadaiwa kuwa kilichukuliwa miezi miwili iliyopita na kusambaa kwake kumeyaamsha mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia wahamiaji.

Video hiyo ilitumwa kwa taasisi ya habari ya France24 Observers ambayo iliripoti na baadaye Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) liliingilia kati na kusaidia watu hao kurejeshwa nchini Nigeria.

“Kama sio ile video tusingeweza kurudi tena Nigeria, ninaamini hivyo,” Efe Onyeka mwenye umri wa miaka 25 aliyerekodi video hiyo ameiambia AFP.
“Walikuwa wanatupiga kwa kutumia mabomba ya chuma, mijeredi na hawakuwa wanatupatia chakula [kwa muda mrefu]. Hakukuwa na maji, tulikuwa tunakunywa maji yanayotoka kwenye mifereji iliyopitisha mikojo,” aliongeza.

Alisema hadi sasa amekuwa akiota na ndoto mbaya akiyakumbuka Maisha ya selo za Libya.


Alisema kuwa alikamatwa katika bahari hiyo alipokuwa anajaribu kwenda Ulaya kwa lengo la kufanikisha ndoto yake ya kucheza mpira wa kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad