Video: Ukinuna, Ukiumia Ukweli ni Wasanii Wanaofanya Vizuri TZ Wanatoka WCB! – Babu Tale

Mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Babu Tale amefunguka kwa kudai kwamba kwa sasa wasanii ambao wanafanya vizuri nchini Tanzania wanatoka katika label yake ya WCB.

Akizungumza na Bongo5 mapema leo, Babu Tale alisema suala la mikataba ya wasanii wao lipo vizuri na hawana mpango wa kuipitia kama baadhi ya wadau wanavyoshauri baada ya kutokea sakata la Rich Mavoko.

“Hatuna mpango wa kupitia mikataba wa wasanii wa WCB, mikataba ya wasanii wetu wote haina matatizo, kama unavyoona wasanii wetu wote wanafanya vizuri,” alisema Babu Tale. “Wasanii wanaofanya vizuri nchini Tanzania kwa kipindi hichi wanatoka Wasafi iko wazi ukinuna ukiumia wasanii wanaofanya vizuri kwa kipindi hiki Wanatoka Wasafi,”


Wiki mbili zilizopita Mkurugenzi wa vipindi EFM, Sebo aliishauri kampuni hiyo kupitia upya mikataba ya wasanii wao kwani kitu ambacho kimetoka kwa msanii Rich Mavoko kwenda kulalamika BASATA hakikuleta picha nzuri kwa taasisi hiyo kubwa ya muziki nchini Tanzania.

Mavoko ameingia kwenye mgogoro na WCB na sasa ameanza kufanya kazi zake binafsi chini ya label yale ya Billionea Kid.

Bongo5

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad