Hatimaye zoezi la kukikwamua kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara na kuua mamia ya watu limekaribia kukamilika baada ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa kushirikiana na wataalam mbalimbali wakitumia tingatinga kukivuta kivuko hicho hadi karibu na mwalo wa Bwisya ambapo kitakabidhiwa kwa TEMESA kwa ajili ya matengenezo.
Kivuko hicho kilianza kuvutwa jana mara baada ya zoezi la kukigeuza kukamilika.
Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika leo Ijumaa Septemba 28, 2018, na baada ya hapo maji yaliyomo ndani yataondolewa na baadaye taratibu za kukikarabati zitafanyika ili kirudi kwenye hali yake ya awali.
Pamoja na mitambo maalum ya kuvuta na kunyanyua vitu vizito, kazi hiyo pia inafanywa na meli kubwa ya mizigo ya MV Nyakibalya ambayo imekibana ubavu wa kulia kivuko hicho ili kisipinduke tena wakati kikivutwa
VIDEO:Tazama Kivuko cha MV Nyerere Kikivutwa kwa Tahadhari
0
September 28, 2018
Tags