Vigogo Kiwanda cha chai Mponde mahakamani kwa uhujumu uchumi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imewafikisha mahakamani vigogo sita wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha wakulima wa chai cha Mponde kwa tuhuma za uhujumu uchumi.

Watuhumiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Tanga, mbele ya Hakimu Desidery Kamugisha na kusomewa mashitaka mawili ya uhujumu  uchumi.

Vigogo hao waliofikishwa mahakamani ni pamoja na  Nawabu Mulla, Shahdadi Mulla, Wiliam Shelukindo, Richard Mbuguni, Richard Madandi na Rajabu Msagati.

Akiwasomea mashitaka mwanasheria wa serikali, Seth Mkemwa akisaidiana na Magulo Waziri, alidai kati ya mwaka 2000 na 2013 watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikula njama na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 30.

Katika kosa la pili kwa watuhumiwa wanadaiwa kuidanganya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutaka msamaha wa kodi katika vifaa mbalimbali walivyodai kuviingiza kwa ajili ya wakulima wadogo wa chai jambo ambalo si kweli.

Aidha watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad