Vikao vya Bunge Vyaanza Leo Dodoma

Vikao vya Bunge Vyaanza Leo Dodoma
Vikao vya mkutano wa 12 wa Bunge vinavyoanza leo jijini  Dodoma vinatarajiwa kupitisha katika hatua zilizobaki miswaada mitano ya sheria ikiwemo Muswaada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Waalim  nchini  wa mwaka 2018.


Taarifa iliyotolewa leo Septemba 3, 2018 na Kitengo cha Hhabari kwa Umma na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, imesema,  miswaada mingine ambayo tayari ilishasomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa 11 ni Muswaada wa Sheria ya Kulitangaza jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018.

Miswaada mingine ni pamoja na wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 2 wa mwaka 2018 muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 wa Mwaka 2018, muswada wa marekebisho ya sheria ya ubia kati ya sekta ya Umma na binafsi wa mwaka 2018.

Pia, mkutano huo utashuhudia kiapo cha uaminifu kwa Mbunge mteule wa Buyungu (CCM) Christopher Chiza aliyechaguliwa Agosti 12, 2018 uchaguzi huo wa Buyungu, ulifanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago (CHADEMA) kufariki dunia Mei 26, 2018 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mkutano huo utakaomalizika Septemba 14 mwaka huu, utakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na wabunge na wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa waziri mkuu ambapo pia kamati ya sheria ndogo itawasilisha taaarifa zake bungeni zinazohusu uchambuzi wa sheria ndogo kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad