Viongozi wa kijiji Wafunga Ofisi Watimka Kisa Operesheni ya Bangi

Viongozi wa kijiji  na Wanakijiji Watimka Kisa Polisi
Wananchi wa kijiji cha Kisimiri juu kilichopo tarafa ya King’ori wilayani Arumeru walikiacha kijiji chao kwa muda huku viongozi wao wakifunga ofisi zao na kukimbia kisa operesheni ya bhangi iliyofanywa na vikosi vya Jeshi la Polisi Alfajiri leo hii.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi amesema kuwa walitapata taarifa kuna kiasi kikubwa cha bhangi kinatarajia kusafirishwa leo ndipo walipoandaa askari hao ambao walifanikiwa kufika eneo la tukio na kupata jumla ya magunia 27 yenye uzito wa Kilogramu 25 kila gunia, shambani kwa mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa pamoja na Misokoto 583 ya Bhangi.

Kamanda Ng’anzi amesema Jeshi la Polisi linawatafuta viongozi wa kijiji cha Kisimiri juu kwa kukiuka agizo la serikali linalomtaka kila kiongozi katika eneo lake ahakikishe kwamba halilimwi bhangi.

“Tunaendelea kuwatafuta viongozi wa kijiji pamoja na kamati zake za ulinzi na usalama na mkondo wa sheria utachukua nafasi kwani wao kama viongozi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha katika eneo lao hakuna biashara yoyote ya Madawa ya kulevya inayofanyika”, amesema Kamanda Ng’anzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa Jeshi hilo mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Elias Mwita amesema kwamba operesheni hiyo sio ya kwanza kufanyika katika eneo hilo na itakuwa endelevu kuhakikisha kwamba zao hilo haliendelei kulimwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad