Wabunge CHADEMA Watoka Nje na Kususia Kiapo cha Christopher Chiza

Wabunge CHADEMA Watoka Nje na Kususia Kiapo cha Christopher Chiza
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametoka ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati Mbunge wa Buyungu, Christopher Chiza (CCM), akiapa.

Tukio hilo lilitokea mapema asubuhi leo wakati baadhi ya wabunge hao wakiwa  ukumbini tayari kwa kuanza kwa kikao cha bunge lakini walitoka kabla Spika Job Ndugai, hajaingia na kisha kuingia baada ya Chiza kula kiapo cha uaminifu.

Hali hiyo ilisababisha viti vya upande wanaokaa wabunge hao kuonekana vitupu huku wakonekana baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Chiza ameapa leo baada ya kushinda ubunge wa Jimbo la Buyungu baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Kasuku Bilago kufariki dunia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad