Amesema huenda kuna sababu mbalimbali zilizopelekea muamko hafifu na kuwataka wananchi kujitokeza kabla ya saa kumi ili kupiga kura.
Waitara amesema hayo mara baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kerezange kilichopo Kivule asubuhi ya leo Septemba 16, 2018.
“Wananchi wanajua zoezi linaisha saa kumi jioni, kuna wengine wanashughuli mbalimbali mi naona zoezi linaenda vizuri hali ni shwari na bado kuna muda wa kutosha wa watu kuendelea kupiga kura…” amesema Waitara
Akizungumza kuhusu tishio la vurugu, Waitara amesema hakuna vurugu kwa sababu wageni waliokuja wakati wa kampeni wameshaondoka waliobaki ni wenyeji.
"Hili ni jimbo letu sisi mwisho wa siku tumebaki wenyewe wajuaji wameshaondoka, hivyo hakuna vurugu.
"Ukumbuke hili jimbo lina mitaa 70 saba tu ndiyo ya upinzani na 63 ni CCM, unaweza kuona ni kwa jinsi gani hakuwezi kuwa na vurugu hakuna anayeweza kuifanyia vurugu CCM," amesema Waitara.
Uchaguzi wa jimbo la Ukonga unarudiwa kufuatia aliyekua Mbunge wa jimbo hilo kupitia CHADEMA Mwita Waitara kutangaza kujivua nafasi hiyo july 28 mwaka huu kwa madai ya kuwa na mgogoro na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.