Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kimataifa ya Hazina, Patrick Cheche na walimu wenzake wanne wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwapa maudhui ya mtihani wa taifa wa darasa la saba watahiniwa wa shule hiyo.
Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo Jumatano Septemba 26 na kusomewa mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono.
Wakili Kombakono aliwaja washtakiwa hao kuwa ni, Mwalimu Cheche, Laurence Ochieng, Justus James, Nasri Mohammed na Mambo Iddi.
Washtakiwa hao wanadaiwa Septemba 5, mwaka huu waliingilia mitihani ya taifa isivyo halali, walipata kwa makusudi wakawaonyesha watahiniwa maudhui ya mitihani hiyo ambapo walikana mashtaka hayo, kesi hiyo itatajwa Oktoba 10 mwaka huu.
Walimu Hazina Mbaroni kwa Kuwapa Wanafunzi Darasa la Saba Mitihani
0
September 26, 2018
Tags