Wanachama Simba Waijia Juu TFF..... Waitaka Itengue Adhabu ya Meneja Wao

Wanachama Simba Waijia Juu TFF..... Waitaka Itengue Adhabu ya Meneja Wao
Baada ya kufungiwa kwa mwaka mmoja pamoja na kupigwa faini ya shilingi milioni 4 za kitanzania kwa Meneja wa timu ya Simba, Richard Robert, Wanachama wa klabu hiyo wamesema wataanzisha mkakati wa kuhakikisha haki inatendeka.

Wanachama hao wamesema kwa sasa mipango yao ni kuhakikisha wanapaza sauti kuanzia kwenye vyombo vya habari ili kuweka mambo sawa mpaka kieleweke juu ya adhabu aliyofungiwa Meneja wao.

Kupitia Radio EFM, Mwanachama aliyewawakilisha wenzake anayejulikana kwa jina la Jose Munyama, amefunguka na kueleza wanaanzisha kampeni ya kimyakimya ili kulishinikiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watengue maamuzi hayo.

Munyama amesema TFF haijatenda haki kwani adhabu hiyo ni uonevu mtupu kwa Robert ambaye wanaamini hakuwa na makosa ya kupewa adhabu kubwa kiasi hicho.

Mwanachama huyo ameongeza kwa kuwataka TFF wakae upya kupitia kanuni na taratibu walizotumia kumfungia Robert kisha waje na majibu mapya ambayo yatakuwa yanaridhisha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad