WANANCHI wa kijiji cha Mapanda wilayani Mufindi mkoani Iringa wamelalamikia kitendo cha kutozwa faini ya shilingi 50,000 katika Kituo cha Afya cha Mapanda kutokana na akina Mama kujifungua Nyumbani mara wanapopatwa na uchungu kwa madai kuwa ni unyanyasaji.
Wakazi hao wamemwelaza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi wakati wa Mkutano wa Hadhara katika ziara yake mkoani humu ambayo inafahamika kwa jina la tarafa kwa tarafa kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Wemesema kitendo cha kutozwa shilingi 50,000 imekuwa ni kero kubwa kwa akina Mama wanapojifungu wakiwa nyumbani kutokana na sababu mbalimbali zilizopelekea kushindwa kwenda kujifungulia kwenye Kituo cha Afya.
Wananchi wa Iringa Walalamikia Kutozwa Faini Elfu 50 kwa Wamama Wanaojifungulia Nyumbani
0
September 12, 2018
Tags