Wanaume Acheni Kuwanyanyasa Wanawake- Nikki wa Pili

Wanaume Acheni Kuwanyanyasa Wanawake- Nikki wa Pili
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili ameitaka jamii ya kitanzania hususan wanaume, kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanawake kwani nao wanastahili kupata heshima kama wapatayo watu wengine katika familia.

Nikki ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii Instagram baada ya kuwepo dhana potofu katika baadhi ya wanaume, kuhofia kuzidiwa kipato, elimu maarifa, cheo na mwanamke pindi wakipata nafasi ya kufanya jambo lao fulani.

"Utakapo zungumza haki za wanawake wa kwanza kuzipinga na kuzijadili ni wanaume na watapinga kwa faida yao na sio kwa faida ya mwanawake. Utasikia mwanamke akipata hela anakuwa na kiburi, vipi mwanaume akipata hela si ndio balaa, kwanza atabadili wanawake kama nguo", amesema Nikki wa Pili.

Pamoja na hayo, Nikki ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa "mwanamke ukimpa uongozi ataharibu hebu tazama dunia anayoiongoza mwanaume ilivyo na mabalaa, vita, rushwa, umasikini, dhuluma, mauwaji. Wanasema baba ni kiongozi ni kusema tu ila ukweli familia nyingi zimedumu kwa kuwa mama kasimama imara baba kuzingua kitu cha kawaida, sisemi mwanamke ni mkamilifu hapana ila tuache sababu zisizo na msingi. Wanawake mkikubali mtabaki wa nyonge na jamii itadumbukia katika shida zaidi".

Kwenye miaka ya hivi karibuni, wanawake wameweza kupata nafuu kidogo katika kupata haki zao za msingi baada ya kutolewa elimu elekezi kutoka kwa taasisi na mashirika mbalimbali yanayotetea haki za wanawake, na kuifanya jamii kuweza kutambua na kuwaheshimu wanawake kwa namna moja ama nyingine licha ya kuwepo baadhi ya maeneo ukandamizwaji wa wanawake kuendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad