Wanawake Ndio Wanaongoza kwa Uchawi- Mbasha

Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha ameitaka jamii ikimee vitendo vya uchawi na ushirikiana hadharani kwa kuwa vitu hivyo vinaenda kinyume na maandiko ya Mungu, huku akidai wanaongoza kufanya hivyo ni wanawake.

Mbasha ameeleza hayo asubuhi ya leo Septemba 07, 2018 kupitia ukurasa wake wa kijamii, baada ya kuwepo wimbi kubwa la jamii kuamini vitendo vya ushirikina na uchawi kuliko kumuelekea Mungu katika kuomba haja zao.

"Biblia inasema, 'usimuache mwanamke mchawi kuishi. (Kutoka 22:18), katika biblia ya  'The Amplified bible' inasema, usimruhusu mwanamke anajihusisha na vitendo vya kichawi au aishi. Sijajua ni kwanini andiko hili limewalenga wanawake wachawi tu na siyo wanaume, ingawa kuna wanaume ambao ni wachawi pia....

Nahisi wakati Musa anaandika kitabu hichi, uchawi ndiyo ulikuwa starehe kubwa ya wanawake wa zama hizo, kama ilivyo leo dhambi kubwa ya wanawake wasiomcha Mungu ni kukesha Instagram huku hawajavaa nguo za kujisitiri na kucheza michezo ya uasherati na kujidai wanajua kila kitu, huku wakiwa na midomo michafu bila kujali 'status' na umri wa watu wanaowatukana. Huu nao ni uchawi tena uchawi wa kisasa", ameandika Mbasha.

Aidha, Mbasha amesema kwamba vitendo vya uchawi ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya watu kwa maana wengi wao huwafanyia wenzao matendo mabaya, kusudi wasiweze kupiga hatua fulani ya kimaisha na wabakie kuhangaika na dunia bila ya kuwa na mafanikio yoyote.

"Unakuta mtu anaomba maombi mabaya ili Mbasha asifanikiwe, huyu ni mchawi tu. Mtu unapiga simu kuharibu 'réputation' yangu ili nisipate 'deal', wewe ni mchawi tu. Mahakama imeniachia huru na kukuta sina hatia halafu wewe bado unaniita mtuhuwiwa wewe ni mchawi tu. Unamchukia Rais Magufuli anaeleta maendeleo wewe ni mchawi tu. Uwe mwanamke au mwanaume mwenye tabia tajwa hapo juu wewe ni mchawi", amesisitiza Mbasha.

Andiko hilo la Emmanuel Mbasha limekuja baada ya ku-trend matukio ya ushirikina na uchawi katika mitandao ya kijamii ndani ya wiki hii, ambayo yana watuhumu wasanii wa filamu na muziki nchini katika ufanisi wa kazi zao.

Dhana na imani ya watu wengi katika ulimwengu wa sasa, huvipa vipaumbele vitendo vya ushirikina na uchawi kwenye kufanikisha masuala yao fulani fulani , ili kusudi waweze kupata majibu ya haraka katika kile wakitakacho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad