Wanawake wa Songwe Wakiri Kuwapiga Waume zao


Wanawake mkoani Songwe, wamekiri kuwapiga waume zao huku sababu za kufanya hivyo zikitajwa kuwa ni mienendo mibaya ya wanaume hasa kutelekeza familia baada ya kuuza mazao, kipindi cha mavuno na wanaume hao wakiona aibu kushitakia katika Dawati la Jinsia.



Wakiongea leo kwenye Dawati la Jinsia mkoani humo, wanawake hao wamesema inawalazimu kufanya hivyo kutokana na kushindwa kujizuia pale wanapokuwa wamekosewa na waume zao.

''Mkishavuna badala ya mazao yawasaidie kusomesha watoto na kujikimu na mahitaji matokeo yake mwanaume anauza na kwenda kutumia fedha na hawala, kwahiyo akirudi unakuwa umechukia unazaba makofi'', ameeleza Joyce Msyani.

Licha ya wanaume hao kutendewa ukatili huo na wake zao imetajwa kuwa ni asilimia ishirini tu ya wanaume wanaojitokeza kutoa taarifa katika dawati la jinsia kwa mkoa wa songwe huku mfumo dume ukitawala miongoni mwao.

Dawati la Jinsia mkoa wa Songwe limedai kuwa asilimia themanini ya wanaume hawaendi kuripti matatizo yao katika dawati hilo kwa kuogopa kudharaulika katika jamii inayowazunguka.

Pamoja na kuendelea kwa vitendo hivyo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanaume mkuu wa mkoa wa songwe Brigedia Nicodemus Mwangela, ameviomba vyombo vya habari kuhakikisha vinatoa elimu mara kwa mara katika jamii ili kumaliza tatizo hilo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad