Waokoaji Walivyotambua Kuna Mtu Bado Ndani ya Meli Iliyopinduka Mwanza


Katika hali isiyo ya kawaida mtu mmoja amepatikana akiwa hai katika kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana karibu na kisiwa cha Ukara baada ya kukaa majini kwa takribani siku tatu.

Kwa mujibu wa waokoaji mtu huyo ametambulika kwa jina la Agustino Charahani ambaye ni fundi mitambo wa kivuko hicho.

Taarifa kutoka kwa mwanishi wetu Sophia Goorge aliyepo, eneo la tukio huko Ukara, fundi mitambo huyo alikuwa amejificha kwenye chumba maalum cha kujihifadhi pindi itokeapo ajali.

Waokoaji wameeleza kuwa tangu MV Nyerere ilipozama juzi mchana mtu huyo alikuwa akipiga kwa kutumia kitu kizito kivuko hicho kuomba msaada.

“Siku ya kwanza wakati tunaokoa watu hatukuweza kusikia vizuri ishara zake za kuomba msaada wa kuokolewa lakini jana jioni tulianza kusikia sauti ya mtu akipiga kitu kwenye kivuko hicho,” alisema mmoja wa waokoaji.

Mtu huyo amepatikana leo majira ya saa tano hata hivyo ameishiwa nguvu na hawezi kuongea na kwa sasa amelazwa katika kituo cha Bwisya kilichopo Ukara kwa matibabu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad