Yerico ameyasema hayo ikiwa leo ni siku ya tatu tangu msanii Maua Sama kuwekwa ndani na pia Soudy Brown kwa kosa la kucheza wimbo wa iokote na kuonekana akiwa anakanyaga noti ya shilingi elfu 10 kitu mabacho jeshi la polisi linasema kuwa ni swala la kudharirisha noti ya Tanzania.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Yerico anasema ” wasanii wa tz kunsdi la wanafiki , huenda kuwazidi hata wanasiasa, siku ya tatu sasa maua sama na Soudy Brown wako mahabusu kwa kosa la cybercrime kuchezesha na kukanyaga pesa lakini wasanii nchini ako kimya kana kwamba hakuna kitu.ngoja twende sie wanasiasa tukawasaidie.