Wasanii Wakaa Uchi Wanatuponza Wasanii Wote- A.T

Wasanii Wakaa Uchi Wanatuponza Wasanii Wote- A.T
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini AT amefunguka na kudai kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao wamekuwa na mtindo wa kukaa uchi mitandaoni hivyo kusababisha taswira mbaya.

AT amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na maisha ya wasanii na kuwashauri endapo wanataka msaada kutoka serikalini hasa kutoka kwa Mhe.Rais basi waache kabisa mambo ya ajabu.

AT amesema hayo huku akitolea mfano wadada wanaokaa uchi mitandaoni na kusema kuwa Mhe. Rais akiytaona hayo ataona hao wasanii ni wahuni tu,kumbe kuna wengine wanaiharibu sanaa yetu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, AT amefunguka haya zaidi:

Rais hawezi kuwa na moyo wa kutusaidia wasanii hata siku moja kutokana na haya mambo ya kiki, Hizi mambo zimekuja kutuharibia kila kitu na zitatuharibia kila kitu sasa hivi ykiwaambia wabunge kuhusu wasanii wenyewe wanawajua sikinde tu kwa sababu wanaona wengine ni wakaa uchi na kutushusha thamani wasanii wote wa kweli ambao tunafanya sanaa”.

Lakini pia AT amekemea matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kusisitiza kuwa lazima watu watumie vizuri mitandao ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad