Wasanii Wanaotengeneza Dola Wakamatwa Dodoma


Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Giles Muroto amethibitisha kukamatwa kwa vijana ambao wanadaiwa kufanya shughuli za kisanii kwa kufyatua noti za dola bandia, ambazo hazina tofauti na dola halisi za Marekani, kitu ambacho ni kinyume cha sheria.


Picha zikionesha matukio mbalimbali wakati Kamanda Muroto akielezea.

Akiongea leo Kamanda Muroto amesema vijana hao watatu, wamekamatwa na mtambo wao ambao wanautumia kufyatua hizo noti bandia kisha kuanza kuzitumia katika maonesho yao.

''Tumewakamata vijana hawa ambao wanafanya usanii wa kufyatua dola ambazo kwa hali ya kawaida mwananchi hawezi kuzitofuatisha na noti za kawaida hivyo vitendo hivi vinalitia aibu taifa'', amesema Muroto.

Akiwahoji mbele ya wanahabari Muroto aliwauliza vijana hao wanafanyeje kufyatua noti hizo ambapo wameeleza kuwa walikuwa wanashusha programu maalum mtandaoni na kuzitumia kutengeneza noti hizo.

Muroto pia amewaonya wasanii ambao wamekuwa wakitumia noti bandia kwenye matamasha yao kwa kuzirusha kwa mashabiki wakati hawana kibali cha kufanya hivyo huku wakijua ni kinyume cha sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad