Wasanii Wengi wa Bongo ni Mastaa na Wana Majina Makubwa Lakini Hawana Pesa Kabisa- Steve RnB

Wasanii Wengi wa Bongo ni Mastaa na Wana Majina Makubwa Lakini Hawana Pesa Kabisa-  Steve RnB
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva na songwriter  Steve RnB Amefunguka na kudai wasanii wengi Bongo ni mastaa na wwana majina makubwa lakini hawana pesa kabisa.

Steve amedai wasanii wengi wanafeli kwa kuwa wanaishi maisha ambayo sio yao kabisa na wanajaribu tu kuishi na hata wakati mwingine msanii anakuwa na jina kubwa Bongo na wakati hana hata pesa.

Kumekuwa na madai mengi kuwa wasanii ambao wanatoa kazi kali ambazo zinapendwa na jamii na hata wanaonekana wakiwa wana magari na hata nyumba nzuri kwenye mitandao ya kijamii mara nyingi wanakuwa wanazima na uhalisia wao ni maisha magumu.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi TV, SteveRnB alifunguka haya;

Wasanii wengi wanafeli kwa sababu wanajaribu kuishi maisha ya kisanii lakini kuna kitu ambacho kinawatupa mkono kwamba umaarufu upo yaani mtu anakuwa maarufu lakini anakuwa hana pesa ambayo inatokana kuwa tulipotoka ilikuwa msanii mziki wake unajulikana sana lakini hamna pesa”.

Wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kabisa kukosa faida ya kazi zao za kisanaa kwani kazi anatoa msanii lakini anayefaidika ni mtu mwingine kabisa lakini hivi sasa tunaona mapinduzi mapya kwenye muzikii wa Bongo fleva kwani wasanii wanapiga kazi na pesa zinaonekana wasanii kama Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Ommy Dimpoz na wengineo wamekuwa na mafanikio zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad