Wasichana wa Mjini Wanaamini Mume Tajiri Anapatikana kwa Waganga – Steve Nyerere

Wasichana wa mjini wanaamini mume tajiri anapatikana kwa waganga – Steve Nyerere
Msanii wa filamu nchini, Steve Nyerere  amedai kuwa wasichana wengi wa mjini wanaamini hawawezi kutusua kimaisha  au kupata wanaume wenye pesa bila kwenda kwa waganga wa kienyeji.

‘’Ninachotaka kuamini mchawi mkubwa ni Mungu peke yake ukimwamini yeye utashinda vitu vingi ikiwemo na huo uchawi, na unaweza kuwasaidia wajinga wachache lakini mimi kwangu naamini ukishirikiana na Mungu utatusua, na wengi wanaofanya uchawi na kuufanya kuwa ni kipaumbele iwe kwenye kazi au maisha ya kawaida hawakai muda mrefu, uchawi ukiisha wanabaki wao kama wao. Mungu hana mwisho ila uchawi una mwisho ila Mungu  ukimwamini, ukamlilia na ukampigia magoti hawezi kukutupa mja wake’’ Alisema Steve Nyerere alipozungumza na mtandao wa Cloudsfm.co.tz

‘’Kuna wengine hawawezi kufanya jambo lolote bila kumwambia mganga hata kwenye mambo ya maendeleo hawataki kuamini kama Mungu yupo, na hii imeingia kwenye akili za wasichana wengi wanaoamini ili kutusua maisha au kwenda nchini China, kuvaa vizuri na kumpata mwanaume mwenye pesa lazima waende kwa mganga.’’ Aliongeza Steve.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad