Wastara Afunguka Kuhusu Kiki za 'Nusu Utupu'

Wastara Afunguka Kuhusu Kiki za 'Nusu Utupu'
Msanii wa filamu nchini, Wastara Juma amesema yupo mbioni kurejea katika ulingo wa sanaa hivi karibuni, huku akidai haitokuja kutokea kwa yeye kuvaa nguo za nusu utupu ili apate 'kiki' mitandaoni kama wanavyofanya wasanii wengine pindi wanapoamua kuachia kazi zao mpya.

Wastara ametoa kauli hiyo alipokua anapiga stori na www.eatv.tv baada ya kuwepo tabia ya wasanii wengi nchini, pindi wanapokuwa wanataka kurejea kwa mara nyingine katika kazi walizokuwa wakizifanya kutengeneza 'kiki' kwa lengo la kutaka kuzungumziwa midomoni mwa watu pamoja na mitandaoni ili kutengeneza njia rahisi ya kupokelewa kazi zao.

"Ninaamini nina mashabiki wamenipenda kama jinsi nilivyo kwa hiyo sidhani mashabiki zangu kama watapenda nibadilike niwe navaa nguo za nusu utupu kusudi nishindane na vijana wa sasa. Binafsi sijafikiria kuishi katika maisha hayo na haitaweza kutokea kwa hiyo nitaendelea kufanya sanaa yangu kama nilivyozoeleka", amesema Wastara.

Pamoja na hayo, Wastara ameendelea kwa kusema "System' yangu ya maisha na uvaaji utabaki ule ule kwasababu sifikiri kutafuta kiki mitandaoni ili ni 'trend' kwa mambo ya kijinga, mimi najua nipo na watu wanaelewa hilo 'so' inatosha kufanya kazi zangu kwa aina hiyo".

Mbali na hilo, Wastara amedai kwa upande wake suala la wasanii kuzuiwa kufanya shughuli za kichama (CCM), haziwezi kumuathiri kwa jambo lolote katika utendaji wa kazi zake kwa kuwa hakuenda kuwaomba kushiriki kuifanyia kazi bali waliombwa kuipa 'support'.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad