Waziri Awaagiza Kukamatwa kwa Watoto Omba Omba na Kuwafikisha Mahakamani

Waziri Awaagiza Kukamatwa kwa Watoto Omba Omba na Kuwafikisha Mahakamani
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Joseph Kakunda amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri chini ya usimamizi wa wakuu wa Mikoa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kuwakamata watoto wote ambao huzagaa mitaani wakiomba omba pamoja na wazazi wao na washtakiwe mahakamani chini ya sheria ya elimu ya mwaka 78 inayokataza utoro.



Naibu Waziri Kakunda ametoa maagizo hayo leo Bungeni katika mkutano wa 12 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kiembe Samaki Zanzibar, Ibrahim Raza na kuwataka wananchi kutumia fursa zilizowekwa na serikali kwa ajili ya kujikwamua na umaskini ikiwemo Elimu bure.



Aidha Naibu Waziri Kakunda amebainisha kuwa ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam imetekeleza hatua mbalimbali za kuwaondoa ombaomba ikiwemo kuwakamata na kuwasafirisha makwao lakini wamekuwa wakirudi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad