Waziri Lugola Aingilia Kati Sakata la Mgambo Kujerui Mwananchi

NA ISMAEL MOHAMED
Wizara wa Mambo ya Ndani ya nchi imefunguka na kulaani vikali vitendo vya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi bila ya sababu yoyote, ikiwemo kupiga, kujeruhi na kupelekea wengine kupoteza maisha.

Hayo yameelezwa na Waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola leo Jumapili Septemba 02, 2018 alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, baada ya kupita siku chache tokea iliposambaa 'video clip' mitandaoni, ikimuonyesha mmoja ya askari mgambo wa jiji akitembeza kichapo kikali kwa mwananchi kwa kile kinachodaiwa kutofanya usafi.

"Suala la mgambo waliowekwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwapiga na kuwajeruhi wananchi limewaondolea sifa ya kuendelea kuwatumikia wananchi, ni vema halmashauri ikatafuta njia mbadala ya kushughulikia suala hilo la usafi na kudhibiti matukio hayo. Hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria nchi hii hivyo tusitoe hukumu na badala yake tuviachie vyombo husika vitimize wajibu wake", amesema Lugola.

Pamoja na hayo, Waziri Lugola ameendelea kwa kusema kuwa "Mahakama pekee ndicho chombo cha kutoa adhabu kwa mujibu wa Katiba na sheria. tutawashtaki wote waliohusika bila kujali vyeo, majina wala umaarufu wao kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria".

Mbali na hilo, Waziri Lugola amewataka watanzania kufuata sheria za nchi zisemavyo, na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vimekuwa vikishamili katika miaka ya hivi karibuni, licha ya wanaharakati wengi kuvipigia makelele lakini kumekuwepo baadhi ya kundi wakivipa kipaumbele vitendo hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad