Rais John Magufuli, amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, kuwakamata na kuwahoji Mwenyekiti wa Kijiji cha Nata na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, baada ya kutuhumiwa kula fedha za mapato za kijiji hicho.
Hayo yamejitokeza leo Septemba 6 baada ya msafara wa Rais kusimamishwa katika kijiji hicho akiwa anatokea Wilayani Bunda, akiwa njiani kuzindua ujenzi wa barabara.
Akiwa katika kijiji hicho, alisimama zaidi ya dakika 20 kusikiliza kero kutoka kwa wananchi, waliolalamikia viongozi wa eneo hilo kufuja mapato ya kijiji.
Hata hivyo majina ya waliorushiwa tuhuma hizo hayakupatikana mara moja.
Baada ya viongozi hao kutajwa, Rais Magufuli aliwaita ili wajitetee lakini hakuridhika ndipo alipomuita Waziri wa Mambo ya ndani, Kangi Lugola akimtaka achukue hatua.
Bada ya kusimama, Lugola amesema:
“Hivyo kwa kuwa tayari hapa kuna tuhuma dhidi ya viongozi hawa, ngoja tuwachukue wakahojiwe kwa ajili ya kujua ukweli wa fedha hizi zinapelekwa wapi.”
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli, ametoa Sh5,000,000 taslimu kwa shule ya Sekondari Nata baada ya wanafunzi kulalamika kuwa na matatizo ya mabweni na vitanda hali inayosababisha kulala wawili kitanda kimoja.
Alikabidhi fedha hizo mbele ya Mkuu wa Shule na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nata, huku akiwaeleza kuwa wataamua waanze na ujenzi wa bweni au kununua vitanda.
“Waziri Lugola Mkamateni Huyu Mpaka Aseme Hela Kaweka Wapi” Rais Magufuli Aamuru
0
September 06, 2018
Tags