Wema Sepetu Azidi Kugombani Jina la Tanzania Sweetheart...Amchana Hamisa Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka n kumnyooshea maelezo juu ya Jina la ‘Tanzania Sweetheart’ na kusisitiza pekee yake anaweza kuwa.

Kwenye mitandao ya kijamii Kumekuwa na mvutano kati ya mashabiki wa Wema na mashabiki wa Hamisa Mobetto ambapo wamekuwa wakigombani Jina la Tanzania Sweetheart na kila mmoja kudai staa wake anastahili kuitwa jina hilo.

Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Wema Sepetu Msanii wa filamu Wema Sepetu aka TZ Sweetheart amedai haoni sababu ya watu wengine kutaka kutumia jina hilo kwa kuwa yeye amekuwa akilitumia kwa muda mrefu baada ya kupewa na mashabiki wake.

Mimi Jina langu ni Wema, Tanzania Sweetheart ni Jina ambalo nimepewa na mashabiki zangu kutokana na mapenzi yao kwangu kwa hiyo hatuwezi kuwa Ma- Tanzania Sweetheart wawili kila mtu Awe na Jina lake halafu kuna Tanzania Sweetheart mmoja tu mbona majina yako mengi jamani”.

Wema na Hamisa wamekuwa Kwenye bifu  ya muda mrefu huku Wema akimtuhumu Hamisa kwa kumsema vibaya kwa watu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad